Kila mmoja anaweza kueleza kwa nyanja yake toufati ya kueleza na hasa ukiangalia sana hakuna kilichofanikiwa katika michezo, hii inatokana na kila mara kubwaga katika mashindano ya kimataifa yaani hata ile ya ukanda wa Mashariki CECAFA
NINI KIMEKWAMISHA
Bila ya kuangalia pembeni soka la Tanzania limefeli kwa kiwango cha ‘Degree’ hii inatokana na uongozi mbovu, tamaa na walioshika madaraka katika soka hawako kimichezo japo ukitaka kusifia japo kidogo utawala wa Leodgar Chilla Tenga alijitahidi sana katika nyadhifa yake japo hakuweza kutoa mazonge yote
Kipindi cha FAT ndio uharibufu wa soka ulianzia huko kulikuwa na migogoro mingi sana japo ukiwauliza watu wa FAT nini kizuri watakwambia watu wa riadha walitoka huko lakini kushiriki kombe la mataifa ya Afrika mwaka 1974 ilikuwa kipindi chao.
Tanzania imekuwa kichwa cha mwendawazimu kushindwa kufanya vizuri na bado lawama zinarudi katika shirikisho lakini nusu zinarudi kwa jamii nzima kwa kutokuwa na utulivu japo shabiki haki zake 3, kushangilia, kuzomea pamoja na kuchangia kadi ya uanachama
KUFELI KWA SIMBA NA YANGA
Utaratibu mbovu wa vilabu hivi unafanya uhakika ukosekane wa kuviamini vilabu hivi kutokana na kutokuwa katika mstari bora hasa majungu pamoja na mipango isiyokuwa na malengo
MAZURI
Uwanja wa taifa umejengwa ndani ya miaka 55 na umezinduliwa na Timu ya Brazil baada ya Tanzania kukubali kichapo cha mabao 5 kwa 1 bao la Jabir Aziz na ndiye mfunguzi wa kufunga goli uwanja huo. Mbwana Samatta licha ya kujikomboa mwenyewe lakini bado ametoka wakati huu wa miaka 55.
Kuzaliwa kwa Azam na kuleta mageuzi ya soka hapa Bongo hii imekuwa faida tangu mwaka 2007 na imekuja 2013 imechukua ubingwa ikiwaacha Yanga na Simba ikibutua macho
MIAKA 55 IMEFANIKIWA AU IMEFELI KIMICHEZO?
Reviewed by Unknown
on
22:34
Rating:
![MIAKA 55 IMEFANIKIWA AU IMEFELI KIMICHEZO?](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjiFEPybJa_v9SODDUZzgmJ7uRuu7Gna5ijpq_mucXovk727HgLfyRB9JZJpbNZmAa3W6iVnd4u1ULmhU1_YDKxw2PSA8YMXXVlIiF4LCbBHokmQQE9dwIo23HQ8QHsEAYrynEFMk2kH5AX/s72-c/533362577.jpg)
No comments: