Wembley ni uwanja wa michezo wa taifa nchini England na umekuwa maarufu kwa mechi kubwa zikiwemo fainali za mashindano mbalimbali ya soka. Uwanja huo wenye uwezo wa kuingiza watazamaji 90,000 unakuja kivingine mwaka 2007 pale ambapo Antony Joshua na Wladimir Klitschko watakutana uwanjani hapo kwenye pambano la kuwania ubingwa wa dunia wa Uzito wa juu
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEixWsf__N75kfNCdgSGU0HaYK9R3hR5mpW3HkDFxboG8nO66ZmGiuT5H5k8OPixPP5AZC0jZqIxauLykrJA1kYr0Igvso9pGPROLNSgl1fpenR-4EB9awiU1kqDGaGEqo3ba-RvGq2Y61_j/s320/nintchdbpict0002890976011.jpg)
Siku ya Jumamosi Aprili 29, 2017 Anthony Joshua atakabiliana na Wladimir Klitschko kwenye pambano la kuwania ubingwa wa dunia wa Uzani wa juu wa IBF, IBO na WBA.
Mara ya mwisho kwa pambano la masumbwi kufanyika uwanjani hapo ilikuwa mwaka 2014 ambapo Carl Froch alimwangusha George Groves kwa KO’. Kampuni ya Matchroom ambayo ni maarufu kwa kuandaa mapambano nchini England tayari imethibitisha kuwa pambano hilo huendWakati marafiki hao wawili wakikutana April 29 mwakani, tayari bingwa wa Dunia wa WBC Deontay Wilder amesema yupo tayari kukipiga na atakayeibuika mbabe kwenye pambano hilo lililobatizwa jina la Titanic. Deontay maarufu (Bronze Bomber) ameshapigana mapambano 37 na kushinda yote ambapo kati ya hayo 36 ameshinda kwa KO.
Antony Joshua mwenye miaka 27, mzaliwa wa Watford England amepigana mapambano 18 na ameshinda yote kwa KO huku Wladmir Klitschko raia wa Ukraine akiwa amepigana mapambano 68 akishinda mara 64 ikiwa ni mara 53 kwa KO pamoja na kupoteza mara nne.a likafikisha mauzo ya tiketi 90,000 au zaid
No comments: